Blog

Januari 22, 2021 22:04um
Wahitimu wapendwa,
461 Maoni

Ninaona tabasamu katika nyuso zenu, wazazi wenu wanawapungia mikono kwa shangwe, wakiwakumbatia kwa nguvu, na ninajua kile ambacho wazazi wenu wanafikiria, moyoni mwao, wanasema hiviā€¦ Hatimaye tumetimiza!

Huenda mnahisi kwamba wazazi wenu hawahitaji kujisifia kwa mafanikio yenu; kwa kuwa ninyi ndio ambao mlikuwa mkisoma kwa bidii kwa ajili ya mitihani; wewe ndiye ulikuwa ukiandika notisi kwa ajili ya maswali, ulisoma vitabu vingi, na kuandika kurasa baada ya kurasa ukijaribu kuwazia majibu ya matihani ambayo huenda yakatokea katika mitihani.

Wewe ndiye uliyeamka asubuhi na mapema,  ukihakikisha kwamba umefanya kazi yako ya nyumbani, umebeba chakula chako, unamkumbusha mama yako kuhusu ratiba ya shule ili akupeleka kwa wakati na pia kukumbuka zile risiti ambazo wazazi wako wametia sahihi.

Ni wewe ambaye ulikuwa unabakia shuleni ili kufanya mazoezi ya mpira wa kikapu, ukifanya mazoezi mengi na kurudia tena mazoezi kuanzia za saa 2:00-4:00 usiku kila siku hadi siku ya Jumamosi kabla ya kucheza, na kusubiria kwa subira zamu yako ukiwa kwenye benchi wakati wengine wanacheza mchezo mzima.

Bila shaka, ni wewe ambaye unafanya mazoezi ya vitendo ya sayansi, ni wewe uliyepeleka daftari na mambo mengine yanayohitajika kwa mwalimu wako wa Kiingereza, uliunda makundi ya majadiliano ya masomo ya aina mbalimbali, na kujifunza mambo mbalimbali kwa ajili ya somo la historia.

Naam, hayo ni mambo ambayo wewe umetimiza, ulivuja jasho, kumbukumbu zako, maksi zako, tuzo zako za kuwa mwanafunzi bora, na kikombe cha ambacho ulipewa baada ya kushinda michezoni.

Lakini ninaamini ulipewa msaada au hata ushauri kidogo. Huenda ulikuwa na tatizo la kuchelewa kuamka hadi pale ambapo unaamishwa au tuseme kwamba kila mara ulikuwa na tatizo la kukumbuka kuchukua nyaraka ambazo wazazi wako wametia sahihi, lakini mtu fulani alikukimbilia na kukupatia.

Inawezekana kuna mtu ambaye alikupeleka kwenye mazoezi na usaili, kukuletea ubao, ngudi, na vitatu vya michezo, naye alikuhudumia au kukufulia nguzo zako zilizochafika kwa jasho ambazo utahitaji kuvaa siku inayofuata.

Ni kweli wazazi wako hawakufanya  mitihani yako, lakini ninakuhakikishia kwamba walikuwa na wasiwasi na huenda walisali kwa ajili yako hadi walipoona matokeo yako. Walihisi homa pale ulipokuwa katika chumba cha mitihani, ama ulipokuwa umeachwa kwenye benchi, bila kuchaguliwa na  kocha.

hayo ndio mambo ambayo wazazi wako hufanya.

Ninauhakika uliona na kutambua mambo hayo, hasa pale unapoona watoto wengine hawana wazazi ambao wanawasaidia, wazazi wenye fadhili ambao wanatumia muda wao kujitoa na kuwafariji wengine.

Na tunapozungumzia kujitoa, wewe umebarikiwa  sana ikiwa wazazi wako wanakupenda, na muhimu zaidi ikiwa wanasali kwa ajili yako. Wanasali kwa ajili yako bila kuacha. kwa kweli, hawawezi kuacha  kusali kwa sababu wanajua hali ulimwengu jinsi ilivyo.

Hivyo, wathamini wazazi wako, waonyeshe upendo usio na masharti,  wape pumziko sasa na pale wanapokuwa wamachoka , ama pale wanapokuwa na mashaka kidogo kuhusu maisha. Umekuwa nao kwa muda wote huo na sasa unaondoka jambo hilo linahuzunisha.

Ninajuaje mambo hayo? Mimi pia ni mzazi.

Jifunze kwa wazazi wanaosali ambao walikabidhi kila kitu kwa Mungu ambaye Mwana wake aliacha mazingira mazuri ya nyumbani kwao, kasha kuja duniani na kudhabihu uhai wake kwa ajili ya wanadamu wote.

Ikiwa huna Biblia, nunua nakala moja ili uweze kusoma na kuielewa vizuri. Kisha soma kwa makini kitabu hicho ambacho kimevunja rekodi ya mauzo, kitabu ambacho kinasimulia hadithi bora ya mahusiano kuliko zote katika historia.

Jitoe zaidi,

Mzazi wako

POST COMMENT

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Hifadhi
Nembo