Kuhusu
Sisi Ni Nani

Hududma ya Nenouzima ni Chombo cha habari ambacho ni mkono wa Chama cha Wamisheneri wa Kibaptisti (BMA) cha Marekani. Nenouzima ipo ili kusaidia makanisa ya Chama cha Wamisheneri wa Kibaptisti katika kutimiza Utume mkubwa kwa kutoa habari za Kristo ili kuzalisha wanafunzi wa Yesu Kristo.

Makao makuu yetu ya kimataifa na kituo cha uzalishaji cha msingi yako katika 611 Locust Street, Conway, Arkansas, Marekani. Pia tuna vituo vya uzalishaji vya kikanda nchini Ufilipino, Ghana, Romania, Honduras Peru, Eli Salivador na Nikaragua.

Umiliki

Huduma ya Habari ya Nenouzima ni huduma ya kimataifa ya BMA ya Marekani. Inamilikiwa na kuongozwa na makanisa yanayohusiana
na BMA, ambayo hukutana kila mwaka kusikia ripoti na kufanya kazi kulingana na idara zake mbalimbali.

Usimamizi

Bodi ya wakurugenzi yenye watu kumi na tano waliochaguliwa na BMA ya Marekani ndiyo inayosimamia kazi ya Huduma ya Nenouzima.
Wafanyakazi wa ofisi ya makao makuu wako chini ya uongozi wa ndugu Donny Parrish, ambaye amekuwa mkurugenzi mtendaji tangu Mei 1, 2017.

Msaada wa kifedha

Msaada wa kifedha kwa Huduma ya Nenouzima hutolewa kwa njia ya sadaka za bure za makanisa ya BMA na kwa watu binafsi ambao ni marafiki wa huduma hii. Kwa kuongezea, Msingi wa Huduma ya BMA, iliyoanzishwa mwaka 1998, imeundwa ili kutoa msaada unaoendelea kupitia usambazi wa gawio la sadaka zinazotolewa kila mwaka kupitia Makanisa.