Mwito na Maono
Lifeword Broadcasting

Tangu mwaka wa 1965, Huduma ya Nenouzima ameshiriki injili kwa kutumia teknolojia ya juu zaidi inayopatikana. Radio ilikuwa ni jambo la msingi kama chomo cha mawasiliano na lugha ya Kiingereza kama lugha peke yake, lakini leo Intaneti imesaidia kupanua huduma yake kwa nchi 121 duniani na lugha 42. Wingu la Nenouzima liliyojengwa litaongeza zaidi huduma ya vyombo vya habari ili kufikia mtu yeyote mwenye kuweza kupata mtandao anaweza kupata na kusikia injili kwa lugha zao wenyewe za mama. Ngonga hapa kusikiliza lugha za Nenouzima na Maeneo Lengwa

click hapa above to Sisi ni nani mantangazo ya lugha

Redio ya Jamii ya Nenouzima
Lifeword Community Radio

Tangu mwaka 2014, huduma ya Nenouzima imesaidia makanisa ya ulimwengu wa tatu kuanzisha vituo vya redio vya masafa mafupi ambazo zinawawezesha kuifikia jamii yao na injili. Katika nchi hizi ambazo watu wengi hutembea karibu kila mahali wanapoenda, wengi wa wale wanaohudhuria kanisa fulani huishi na kufanya kazi ndani ya maili 3 au 4-eneo ambalo hufikiwa kwa urahisi na transimita yetu ya ukubwa wa wati 15 za FM ambayo inaweza kutumika na betri ya gari ya volt 12. Huduma ya Nenouzima pia huenda vijijini kuanzisha redio na kisha kufundisha mchungaji na viongozi wa kanisa ili kuanzisha kituo cha redio kwa njia ambayo jamii inapendelea. Huduma ya Nenouzima Katika jamii husika huelezea programu inazozitoa, wao hufanya ushuhudiaji wa mara kwa mara na wa neema juu ya upendo wa Yesu Kristo kwa watu. Watangazaji hao wapya wanakubaliana kusaidia makanisa mengine kufanya kitu kimoja. Tunakiita “Mafunzo ya vyombo vya habari” yalianza.

Wingu la Neno Uzima
Lifeword Media & Leadership Training

Mpango wa hivi karibuni na unaoendelea wa Lifeword unahusisha kujenga jukwaa, Wingu, ambayo itawezesha zaidi ya miongo mitano ya programu za injili kupatikana kupitia mtandao. Lifeword.org itakuwa mahali ambapo mtu yeyote anayesema lugha ya Nenouzima anaweza kusikia kuhusu upendo wa Yesu kwa watu wote katika lugha ya moyo wao.

Lengo kuu ni kwamba lugha 200 za dunia zitawekwa kwenye Wingu na kwamba wasemaji wa lugha hizo wataisikia hadithi kubwa zaidi iliyosimuliwa.

Wingu la Neno lina uwezo usio na ukomo wa kufikia mabilioni kwa ajili ya Kristo.