Blog

Agosti 14, 2018 11:33mu
Radio ya jamii ya Nenouzima ni nini?
780 Maoni

Kuna makundi ya watu 16,000 ulimwenguni, na 7,000 kati yake yanasemekan kuwa “hayajafikiwa” na Injili. Kundi la watu linalojulikana kama halijafikiwa na Injili halina taasisi yoyote ya Wakristo wanaoonesha kuwa na uwezo wa kuwafikia kwa njia ya upandaji wa makanisa. Kwa kwa maana hiyo inamaanisha chini ya asilimia 2 wamesikia jina la Yesu. Lengo la Nenouzima limekuwa daima ni kutafuta makundi ya watu hao na kuwafikia na injili kupitia mawimbi na teknolojia zote zilizopo.

Mwaka wa 1965 Huduma ya Saa ya mavuno (kama hududuma ya Nenouzima ilivyoitwa kwa karibu miaka 30) ilianza programu yake ya injili kutumia kituo cha redio cha Mtakatifu Louis. kwa kutumia vituo vya redio vilivyokuwepo “vikubwa” vilivyokuwa vinatumia masafa makubwa ndo huduma ilianzia hapo kwa karibu miaka minne. Kiongozi wa BMA pamoja na timu ya Nenouzima walianza kufikiria juu ya “kupunguzwa” kwa matumizi kwa kutumia masafa makubwa, kuanza kwa kutumia vifaa vya gharama nafuu ambavyo kwasehemu nyingi, haikuhitaji leseni ya serikali. Mara antena ikawekwa kutoka sehemu ya juu katika kijiji, kwenye kanisa, juu ya mlima, ambapo matangazo yanaweza kusikilizwa katika eneo la kilomita tano hadi saba. Katika kijiji kidogo ambako watu wanaishi na kufanya kazi ndani ya umbali huo, imeonyesha kuwa ni chombo cha injili cha ajabu kwa wachungaji wa wenyeji, makanisa, wapanda makanisa na wamishenary.

Kutokea mwanzo wake mwanzo wa kuchapisha faili za audio za mp3 za Biblia ya Kekchi Biblia iliyokuwa inasomwa katika kijiji cha kijeshi cha Guatemala kutoka kanisa la karibu la Kekchi, wazo hilo limechukua mizizi kwamba vituo vya vya redio vya Nenouzima mpaka sasa vimeenea katika nchi za Chile mpaka Mexico, kutoka pwani ya magharibi ya Liberia hadi Afrika hadi Tanzania, na Asia kutoka Cambodia hadi milima ya mbali ya Ufilipino. Makanisa na wamishenari wa BMA sasa hutumia NenoUzima kukugusa maisha ya watu kwa njia ambazo wachungaji na wamishenari wanasema wasingeweza bila kuwa na redio.

Viongozi wa maono wa Nenouzima duniani kote (angalia majarida ya Aprili, Mei na Juni) wanatafuta daima makundi ya watu ambao hawajafikiwa wanaohitaji mafundisho ya Nenouzima, na baadhi yao hawajawahi kusikia Injili katika lugha zao zao za kuzaliwa.Wakati mwingine huduma yao inakumbwa na matatizo kama mafuriko ya mito wakati wa masika, misitu yenye mbu waambukizao magonjwa, barabara za matope, vichaka vya milima ni mingi, usafiri usio wa uhakika na hali ya hewa isiyo nzuri. Viongozi hawa huwasiliana na wachungaji katika maeneo husika au makanisa ambao hulipa $ 350 kwa ajili ya kupata vifaa vya Neouzima, ambayo ni sehemu muhimu ya mchakato: Ikiwa wata “miliki”, wao watapenda kuvitumia zaidi.

Kisha, kwa mfano ukamilifu wa mchakato wa kuzalisha, viongozi wa maono hutambua, kufundisha, na kufundisha viongozi wengine katika ufungaji, matengenezo na uendeshaji wa vituo vipya vya redio katika maeneo yao ya huduma. Watumishi wanaume kwa wanawake watawafundisha wengine kufanya hivyo. Sehemu ya mwisho ya mchakato hukamilika baada ya mafunzo, lakini huduma ya Neno Uzima daima inaendelea kwa sababu ya sadaka inazopewa.

Kwa sasa kuna vituo takribani 60 hivi viko hewani. Walio wengi wana uwezo wa kufanya kazi bila leseni, lakini sio wakati wote. Vituo vitatu (ambavyo tunavijua) viko katika hatua za mwisho za kupata rasmi leseni na mamlaka za mawasiliano za serikali za nchi husika.

Redio ya Jamii ya Nenouzima inafikia makundi ya watu ambayo hajafikiwa na injili. Mwaka ujao, Mawimbi ya Nenouzima, hifadhi ya mafundisho tuliyo nayo na vifaa vya ufundi, vitakuwa wazi kwa kila mtu yeyote aliye na mpango wa kufikia watu katika lugha lugha za wenyeji. Ukisoma Katika jarida letu litakalofuata utaona, maono na jitihada zinazoendelea kwa mawimbi/ Mtandao zitasisitizwa zaidi.

POST COMMENT

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Hifadhi
Nembo