Blog

Agosti 14, 2018 12:11um
Garifuna: Lugha ya Nenouzima na ya Kabila la Watu
984 Maoni

Timu ya sifa na kuabudu katika kanisa la Garifuna inayoitwa “Iglesia Bautista Nazareth”
Wameanza Ibada yao huko Honduras.

Watu

Watumwa wa Afrika walivumilia safari ya hatari, ambayo mara nyingi ilimalizika kwa kifo na mara nyingi kilisababishwa na magonjwa. Mwishoni mwa mwaka wa 1700 kilikuwa kilele cha biashara ya watumwa wa Trans-Atlantic na kuanguka kwa meli ilikuwa sababu nyingine ya vifo hivi, lakini hadithi ya kabila la watu wa Garifuna, ilikuwa ya kusikitisha, ilihusu maisha … ya aina ya milele

Mnamo 1797, kikundi hiki cha Afrika Magharibi kilipelekwa Honduras na serikali kutoka kisiwa kidogo cha Caribbean kinachoitwa Saint Vincent. Miaka 70 hivi kabla, walikuwa wamezungukwa kutoka nchi za Nigeria, Kongo na Ghana na kuwekewa meli mbili za watumwa wa Kihispania zilizowekwa kwa ajili ya mashamba katika “Dunia Mpya.” Hata hivyo, safari yao iliishia karibu na kisiwa cha West Indies cha Saint Vincent wakati walipoharibikiwa na meli na walipaswa kuogelea kwaajili ya kuokoa maisha yao.

Mara baada ya kufika, waathirika walijiunga na kundi la watu wa Carib na wakajaribu kuepuka kugunduliwa na Waingereza, ambao walidhibiti kisiwa hicho. Lakini mwaka wa 1796, Wagarifuna walijisalimisha kwao, na wafungwa waliwaweka jela ambapo wengi walikufa kutokana na magonjwa. Mwaka mmoja baadaye, walitolewa kwa serikali ya Honduras na kuruhusiwa kukaa huko na kwenye visiwa vya jirani.

Lugha ya Kigarifuna

Zilipopita karne mbili hadi mwaka wa 1980 wakati Mimishenari wa BMA David Dickson na familia yake walipokuwa likizo kwenye Pwani ya Atlantiki, kama saa moja hivi kutoka nyumbani kwao. walikuwa na mapumzika katika pwani,Mara waliwasikia vijana wawili wakiongea kwa lugha ambayo hawajawahi kuisikia. kama kawaida Daudi alizungumza nao kwa lugha ya Kihispania, akajifunza kuhusu Kabila la watu waitwao Wagarifuna.

Mungu aliweka mzigo moyoni mwake juu yao, na kufanya utafiti wake juu ya Wagarifuna wakampeleka kwenye maktaba ya kitaifa ya Belize ambapo alipata kamusi ya Kiingereza-Kigarifuna na kunakili kurasa zake. Kazi yake ya pili ilikuwa kwenda Guatemala na Taasisi ya Wycliffe ya Lugha ambapo alikutana na Lillian Howland, ambaye alimwelezea kuhusu maamuzi yake juu ya kabila hili la watu.

Katika kipindi cha miaka miwili baada ya kukutana na Lillian, alimpa uelewa a kutosha juu ya lugha hii na kumfundisha kusoma, kusema na kuhubiri katika lugha hii isiyo ya kawaida ambayo haikuwa na alfabeti, hakuna rekodi iliyoandikwa,na haikuwa Biblia.

Kigarifuna ni lugha ya moyo ya watu hawa, na wazee, ambao hawajui kusoma na kuandika, hawakuwa na na maandiko yoyote yaliyoandikwa katika lugha hii. Watoto wadogo hujifunza Kihispania wanapokuwa shule na kuwa na lugha mbili, lakini njia pekee ya kufikia watu wazima katika kabila hili na injili ilikuwa ni kuhubiri kwa Kigarifuna na kuwafundisha kusoma, kwa kuanza na Biblia.

Injili

Mnamo Septemba 1982, ndugu Daudi alihubiri hubiri lake la kwanza Ugarifuna na kijana mwenye umri wa miaka kumi na mbili aliokolewa. Ujumbe wake kwa Wagarifuna ulikuwa ni kwamba “Yesu anaweza kuzungumza na kuelewa lugha yako, utamaduni wako na mahitaji yako.” Tangu wakati huo Wagarifuna wengi wametoa maisha yao kwa Kristo, wamefundishwa na kuwafundishwa, na wamepanda makanisa mengi huko Hondurasi. Mahubiri na mafundisho ya Daudi yameandikwa na kuhifadhiwa kwa kumbukumbu na huduma ya Nenouzima, na bado hutumiwa kwenye mafunidsho ya sasa yaliyozalishwa katika kabila la Kigarifuna

Lugha tano tu zimechaguliwa na huduma ya Nenouzima kama “lugha za mwanzo” zilizojumuishwa kwenye hatua ya kipimo kinachojulikana kwa jina la beta kabla ya kuingia kwenye Redio ya Umma ya lifeword.org mpya mwezi Agosti … na moja ya lugha hizo ni Kigarifuna. Kuamua lugha bora zaidi za kutumia, wafanyakazi wa Nenouzima wanazingatia sifa zifuatazo kuhusu matangazo:

Je! Huzalishwa tu na watu wa wasiojua kusoma na kuandika?

  • Je! Ubora ni bora, una maana ya sauti ya kibiblia na ya kiutamaduni husika?
  • Je, kuna tofauti katika muundo, kama vile muundo mrefu na muundo mfupi, na video?
  • Je, wanatumia vyombo vya habari mbalimbali, kama redio za mtandaoni na redio za jamii?

Matangazo ya katika lugha ya Kgarifuna yanaweza kujibu ndiyo katika maswali hayo yote. Shukrani kwa mzigo Mungu aliompa ndugu David Dickson miaka 36 iliyopita, wengi wa watu hawa waliofungwa kwa utumwa sasa wana uhuru mpya na maisha mapya katika Kristo.

POST COMMENT

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Hifadhi
Nembo